TANGAZO


Saturday, March 3, 2012

Airtel, Rotary Club na Usalama barabarani wabandika machapisho kwenye magari

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Balozi Kagasheki (wa tatu kutoka kulia mwenye miwani), akishirikiana na viongozi wa Usalama barabarani pamojana viongozi wa Club ya Rotary ya Dar es Salaam kubandika machapisho ya Usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel kwa kushirikiana na Club ya Rotary yenye ujumbe wa kuhakikisha kuwa madereva wanaendesha kwa usalama zaidi bila kutumia simu za mkononi. Kushoto ni Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga, mwakilishi wa Club ya Rotary, Dar es Salaam, Zainul Dossa pamoja na Hamza Kassongo. (Picha na Mpigapicha wetu)


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Balozi Kagasheki, akishirikiana na viongozi wa usalama barabarani, akibandika  machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na Kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na Club ya Rotary ya Dar es Salaam. Kulia ni Kamanda wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama barabarani, Mohamed Mpinga, na kushoto ni Afisa uhusiano wa kampuni ya Airtel, Jane Matinde akishuhudia zoezi hilo.


  Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama barabarani Mohamed Mpinga, akibandika machapisho ya usalama barabarani ambayo yamedhaminiwa na kampuni ya simu ya Airtel kushirikiana na  club ya Rotary  yenye ujumbe wa kuendesha + simu = kifo, kuhakikisha kuwa madereva wanaendesha kwa usalama zaidi, kulia ni Ofisa Uhusiano wa Airtel, Jane Matinde akishuhudia zoezi hilo.



Afisa uhusiano wa Kampuni ya Airtel, Jane Matinde, akionesha moja ya chapisho hilo, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika zoezi hilo.

No comments:

Post a Comment