Waziri wa Michezo wa Brazil ametangaza kuwa serikali yake haitaki kushirikiana na Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valcke, baada ya malalamiko yake, ambayo alisema hayakubaliki.

Rais wa soka Brazil (kushoto) na Ronaldo nazario mbele na nembo ya Kombe la Dunia Brazil
Bwana Valcke alilalamika juu ya matayarisho ya Brazili ya Kombe la Dunia la mwaka 2014.
Aldo Rebelo alisema hayo baada ya Bwana Valcke kusema kwamba Brazil inaonesha kushughulishwa zaidi na kushinda Kombe la Dunia, kushinda kuitayarisha nchi kwa mashindano hayo.
Alisema ujenzi wa viwanja vya michezo, miundo mbinu ya usafiri na mahoteli kwa ajili ya washabiki, umezorota na kwamba Brazil inahitaji kupiga teke tako, izindukane.
Bwana Rebelo alisema maneno hayo yanakera, na hayalingani na tathmini njema ya awali iliyotolewa na FIFA.
Waziri huyo aliongeza kusema kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana na FIFA - lakini siyo na Bwana Valcke.