Wafanyakazi wa Kampuni ya ENSOL (T) LTD, wakiingia kwenye viwanja vya Hoteli ya Kunduchi, kwa ajili ya bonanza lao la kutimiza miaka 10 ya kampuni hiyo jana Februari 4, 2012. (Picha na Khamis Mussa)
Watoto na wafanyakazi wa kampuni ya ENSOL, wakicheza muziki katika bonanza hilo jana.
Wafanyakazi wa ENSOL, wakicheza wa wavu katika bonanza hilo
Wafanyakazi wakicheza mchezo wa kuvutana kwa kamba katika bonanza hilo
Moja ya timu zilizokuwa zikivutana kwa kamba wakiwa wameanguka chini baada ya kuzidiwa na wapinzani wao.
Wafanyakazi wakikimbia kwa ajili ya kwenda kukimbiza kuku katika bonanza hilo.
Mmoja wa wafanyakazi aliyejishindia kuku, akimuhifadhi kuku wake kwenye begi lake la nguo.
Mmoja wa wafanyakazi alijishindia kuku, akionesha furaha yake baada ya kuweza kumkamata na kuwa wake.
Baadhi ya wanafunzi wa Ujerumani wanaosoma Musoma Chuo cha African Inland Charch of Tanzania (AICT), Musoma, wakimwangalia kuku waliyejishindia kwenye bonanza hilo.
Wafanyakazi wa ENSOL, wakijipatia chakula kwenye bonanza hilo.
Ilikuwa ni wakati wa msosi hapa wafanyakazi na wageni waalikwa wakijipatia chakula cha mchana kwenye bonanza hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa wamejipumzisha kwenye bwawa la kuogelea baada kushindana katika kuogelea kwenye bonanza hilo.
Rahma Kashushu akimfundisha mtoto wake Asumin Kashushu (2), kuogelea, wakati wa bonanza hilo.
Msanii Michael Jackson wa Tanzania, akiburudisha katika bonanza hilo.
Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya ENSOL, wakicheza ngoma kwenye bonanza hilo.
Watoto wa wafanyakazi wa ENSOL, wakishindana katika wakiserebuka kwenye bonanza hilo.
Wafanyakazi wakiserebuka na ngoma ya mduara kwenye bonanza hilo.
Haya tena, haya ndio mambo ya mduara, wafanyakazi wakijimwaya mwaya katika bonanza hilo.
Watoto na wafanyakazi wa ENSOL, wakizirudi ngoma kwenye bonanza hilo.
Baadhi ya wafanyakazi wakijipumzisha baada ya kuserebuka kwenye bonanza hilo.
Babylynn Abby (katikati) wa Shule ya Kimataifa ya East Africa, akipozi kwa picha na baadhi ya wanafunzi wenzake wa shule ya Awali, wakati wa bonanza hilo.
Wanafunzi wa AICT, Judith Komoschinski (wa pili kushoto) na Janna Schinn, wakiwa pamoja na marafiki zao kwenye bonanza hilo.
Mkurugenzi wa ENSOL, Hamis Mikate, akimkabidhi taa ya Sola, Tumaini Samson baada ya kushinda mbio za kuku katika bonanza hilo.
No comments:
Post a Comment