Waziri wa mafuta wa Iran amekariri kuwa nchi yake itaacha kusafirisha mafuta kwa baadhi ya mataifa ya Ulaya, hata kabla ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya mafuta ya Iran kuanza kutekelezwa mwezi wa July.
Alisema kutakuwa na mtafaruku katika masoko ya mafuta ya kimataifa, ikiwa mafuta ya Iran yatasusiwa.
Umoja wa Ulaya na Marekani hivi karibuni, ziliweka vikwazo vipya vikali dhidi ya Iran, wakiishutumu kuwa inatengeneza silaha za nuklia, kisirisiri.
Iran inasema mradi wake wa nuklia ni wa amani.
No comments:
Post a Comment