Chama tawala cha Afrika Kusini, ANC, kimeamua kutekeleza uamuzi wa awali wa kusimamisha uanachama wa kiongozi wa tawi la vijana la chama, Julius Malema.
Wafuasi wa Malema
Hata hivo, kamati ya rufaa ya chama imeamua kuiomba kamati ya maadili kuzingatia tena muda wa kumtoa Bwana Malema chamani.
Kamati hiyo imesema inampa Bwana Malema fursa ya kujitetea tena kama anaona adhabu aliyopewa ni kubwa mno.
Uamuzi wa kumtoa katika chama kwa muda wa miaka 5, ulifikiwa mwezi Novemba, baada ya kukutikana kuwa ameleta aibu kwa chama, kwa kumuendea kinyume Rais Zuma; na kutoa wito kuwa serikali ya Botswana, nchi jirani, inafaa kubadilishwa.
Bwana Malema ameushutumu uongozi wa ANC kuwa unawadharau maskini wa Afrika Kusini, ambao ndio waliompatia ushindi Rais Zuma kwenye uchaguzi.