Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Precision Air, Alfonse Kioko, wadhamini wa safari ya timu ya Golfu ya Gymkhana, akizungumza na wachezaji pamoja na viongozi walioandamana na timu hiyo, wakati wa kuiaga ikielekea nchini Afrika Kusini, leo jioni, Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere, Dar es Salaam kabla ya kupanda ndege, kwa safari hiyo. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mwenyekiti wa Gymkhana Golf Club, Dioniz Malinzi, akizungumza katika hafla ya kuiaga timu hiyo, iliyokuwa ikielekea Afrika Kusini kwa michezo ya kujiimarisha, ambayo itakamilika siku ya Jumapili kwa kucheza na timu mbalimbali za huko. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Precision Air, wadhamini wa safari hiyo, Alfonse Kioko.
Kiongozi wa msafara huo, General mstaafu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mirisho Sarakikya, akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Gymkhana Golf Club, Dioniz Malinzi.
Baadhi ya wachezji wa timu hiyo, waliondoka leo jioni kwenda nchini Afrika Kusini, wakiwa katika hafla ya kuwaaga uwanjani hapo, leo jioni.
Baadhi ya wachezji wa timu hiyo, waliondoka leo jioni kwenda nchini Afrika Kusini kwa michezo ya kujiimarisha na timu za huko, wakisikiliza maelezo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na viongozi wao katika hafla hiyo.
Kiongozi wa msafara huo, General mstaafu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mirisho Sarakikya, akitakiana kheri na Kapteni wa timu hiyo ya golf, Joseph Tango.
Kiongozi wa msafara huo, General mstaafu wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Mirisho Sarakikya, akifurahia jambo na Kapteni wa timu hiyo, Joseph Tango, mara baada ya kuwaaga leo jioni.






No comments:
Post a Comment