Katibu Mkuu wa Liverpool Sports Family (LSF), Ramadhan Said, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mkutano wa mashabiki wa timu hiyo, utakaofanyika kwenye ukumbi wa Meeda Club, Mwenge jijini siku ya Jumapili mchana. Katikati ni Mkurugenzi wa Michezo wa LSF, Seleman Mathew na Mjumbe wa LSF, Mimis Butamu. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mkurugenzi wa Michezo wa Liverpool Sports Family (LSF), Seleman Mathew, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati walipozungumza nao kuhusu kundi hilo na shughuli zake nchini pamoja na mkutano wao, ambao utafanyika kwenye ukumbi wa Meeda Club, Mwenge jijini, ambapo waliwataka mashabiki wa timu hiyo nchini kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo. Katikati ni Katibu Mkuu wa LSF, Ramadhan Said na kushoto ni Mjumbe wa LSF, Said Khamis. (Picha na Kassim Mbarouk)
Viongozi wa Liverpool Sports Family, Mkurugenzi wa Michezo, Seleman Mathew (katikati), Katibu Mkuu wa LSF, Ramadhan Said (kushoto) na Mjumbe wa LSF, Hamis Butamu, wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo asubuhi.




No comments:
Post a Comment