TANGAZO


Sunday, February 5, 2012

Dk. Bilal Mgeni rasmi Maadhimisho ya Kuzaliwa Mtume Muhammad (Maulid)

 Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, akitoa mawaidha katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo, Februari 5, 2012. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Said Sadiki (kulia), akiwa na baadhi ya Masheikh kwenye maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.


 Mgeni rasmi, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kushoto), akiwa na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (wa pili) kwenye maadhimisho hayo.



 Umati wa waumini wa Dini ya Kiislamu, ukiwa katika maadhimisho hayo, viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.



 Wanawake waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa Viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye maadhimisho hayo.


 Wanafunzi wa Madrasatul Alfarouq ya Temeke, Mikorosheni, wakipiga dufu katika maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad (Maulid), Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.


 Wanafunzi na Maustaadhi wa Madrasatul Al-Farouq ya Temeke Mikorosheni, wakicheza dufu wakati wa maadhimisho hayo, Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.


 Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi ( wa pili kushoto), Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal (wa tatu), Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kushoto), wakiwa katika kisimamo (kiamu), kwa ajili ya kumswalia Mtume Muhammad (SAW), wakati wa kuaadhimishwa kuzaliwa Mtume Muhammad,  Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini juzi usiku.


 Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kushoto) na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, wakiwa katika maadhimisho hayo.


 Ustaadh Abdallah Rajab, akisoma mlango wa sita wa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini usiku wa kuamkia leo.


 Mshindi wa tatu wa kuandika makala za kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Ali Asaa, akikabidhiwa zawadi ya sh. 80,000 pamoja na cheti na Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, akipewa zawadi ya Msaafu wa Qur'an Tukufu (kushoto) na mgeni rasmi katika maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad (Maulid), Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia), wakati wa maadhimisho hayo, viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini usiku wa kuamkia leo, Februari 5, 2012. Katikati ni Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, ambaye naye alikabidhiwa wa kwake.

No comments:

Post a Comment