TANGAZO


Tuesday, February 7, 2012

Airtel yakabidhi vitabu kwa Shule 4 za Sekondari Manyara

Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Kampuni ya Airtel, Jane Matinde, akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Yaeda, Ampa  Mary Genda na pamoja na wanafunzi  wa shule hiyo, vitabu   vilivyotolewa na kampuni hiyo kwa ajili ya shule za sekondari nne za Mkoa wa Manyara ambazo ni Yaeda Ampa, Yaeda Chii, Naberera na Merelani Benjamin Wiliam Mkapa, chini ya mpango wake wa shule yetu katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki hii. (Picha na Mpiga picha Wetu)

 Afisa Uhusiano wa Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel, Jane Matinde, akikabidhi vitabu kwa Ofisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Mbulu, Mikaeli Hadu, kwa niaba ya Shule nne za Sekondari, zilizokabidhiwa vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi milioni moja kwa kila shule. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Harry Sinjela.






Wafanyakazi wa Airtel, Wanafunzi, walimu na viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu, mkoani Manyara, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Airtel kukabithi vitabu kwa shule 4 za sekondari zilizopo mkoani hapo.Kushoto waliokaa ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na wa pili ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Harry Sinjela.

No comments:

Post a Comment