TANGAZO


Tuesday, February 7, 2012

Yaliyojiri Bungeni leo


  Naibu waziri , Ofisi ya Waziri mkuu Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Aggrey Mwanri  akitoa ufafanuzi wa maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wabunge  kwenye ofisi ya Waziri Mkuu, yakiwemo masuala ya migogoro ya mipaka ya viwanja kwenye Halmashauri  na Manispaa ya Kigoma –Ujiji pamoja na suala la kuongeza madaktari bingwa na manesi katika manispaa ya Dodoma kufuatia ongezeko la watu na vyuo mbalimbali leo mjini Dodoma. (Picha na Aron Msigwa - Maelezo)


 Mawaziri na wabunge wakifuatilia kwa makini mkutano wa sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, mjini Dodoma. Kutoka kushoto ni Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, mbunge wa Songea, Jenista Mhagama na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samweli Sitta (kulia), wengine waliokaa nyuma ni Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu, Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Naibu waziri wa Kazi na Ajira, Makongoro Mahanga.



 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa ufafanuzi kwa wabunge leo, mjini Dodoma baada ya kuzuia hoja ya mgomo wa madaktari bingwa kujadiliwa Bungeni, hoja iliyoibuliwa na mbunge wa Mbozi Magharibi, Godfrey Zambi  na kufafanua kuwa suala hilo tayari limeshaanza kufanyiwa kazi na Bunge ikiwemo kuiagiza kamati ya huduma za jamii kulifuatilia suala hilo kwa kukutana na pande zinazohusika  na kupeleka majibu bungeni.


 Raia wa kigeni ambao wako nchini  wakiwa ndani ya Bunge wakifuatilia kipindi cha Maswali na majibu cha mkutano wa sita wa Bunge kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda.


Wafanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Taifa) wakitekeleza majukumu yao  ndani ya ukumbi wa Bunge kwa kuhakikisha kuwa watanzania wanayapata matangazo ya Bunge kupitia TBC Taifa moja kwa moja kutoka mjini Dodoma. (Picha na Aron Msigwa –MAELEZO)

No comments:

Post a Comment