Mchezaji Benedict Ngassa wa Moro United (kulia), akimtoka Shadrack Nsajigwa wa Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, leo jioni. Timu hizo zilimalizana nguvu kwa kufungana mabao 2-2. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mchezaji Keneth Asamoah wa Yanga, akipiga mpira kuelekea golini wa Moro United, mpira uliozaa goli la kwanza la timu hiyo, huku Gideon Seppo wa Moro United akijaribu kumzuia bila mafanikio.
Keneth Asamoah (wa pili kulia), akipongezwa na Davies Mwape baada ya kufunga goli la kwanza kwa timu yake.
Mchezaji Simon Msuva wa Moro United, akimchagua golikipa wa Yanga, Shaaban Kado, wakati alipokuwa akifunga goli la pili la timu yake hiyo, uwanjani hapo.
No comments:
Post a Comment