TANGAZO


Saturday, January 21, 2012

Muslim Brotherhood yashinda Misri

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa wabunge wa Misri yametangazwa.

Wafuasi wa Muslim Brotherhood

Yanathibitisha kuwa chama cha Muslim Brotherhood ndicho kilichopata viti vingi kabisa.
Tume ya uchaguzi ilisema kuwa chama hicho kimepata asili-mia-38 ya viti vya vyama, na karibu asili-mia-50 ya viti vyote.
Chama cha Kiislamu cha msimamo mkali kilikuwa cha pili, na hivo kuvipa vyama vya Kiislamu, karibu thuluthi-mbili za viti vya bunge.
Uchaguzi huo uliofanywa katika duru tatu, ndio wa kwanza, tangu Rais Mubarak kulazimika kung'atuka baada ya maandamano.

No comments:

Post a Comment