TANGAZO


Saturday, January 21, 2012

Mamia wamuaga Sumari, wakiongozwa na Rais Jakaya Kikwete

Rais Jakaya Kikwete, akiongoza wananchi kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, marehemu Jeremiah Sumary leo kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam. Sumary atasafirishwa kesho kwenda kwao Arumeru Arusha, kwa mazishi yatakayofanyika Jumatatu. (Picha na Ikulu)

Mwenyekiti wa CHADEMA , ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freman Mbowe, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi wakotoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Sumary.

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, akipita kutoa heshima za mwisho, huku akifuatiwa na viongozi wengine.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa (mbele) akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Sumary.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Konyagi Tanzania, David Mgwassa, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Sumari.

 

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye foleni wakisubiri kutoa heshima za mwisho

JK akiwa na baadhi ya viongozi wakati wa kuuaga mwili wa marehemu Sumary kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam
.

Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa akisalimiana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kwenye masiba huo

Mmoja wa walemavu akiwa amebebwa akiondoka baada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Sumary
JK akimfariji Mjane wa marehemu Sumari, Miriam

Askari wa Bunge, wakiingiza jeneza la mwili wa marehemu, Sumary likiwekwa kwenye gari baada ya kutolewa heshima za mwisho
Mjane wa marehemu Sumary, Miriam

No comments:

Post a Comment