TANGAZO


Tuesday, January 17, 2012

Wananchi wengi wajitokeza kuuaga mwili wa Regia Mtema


Askari wa Bunge wakilibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Regia Mtema, wakilipeleka kwenye gari baada ya kuagwa kwenye viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam leo asubuhi. Maiti imesafirishwa kwenda kwao Ifakara, Morogoro kwa mazishi. (Picha na Richard Mwaikenda)

Askari wa Bunge wakiliingiza jeneza lenye mwili wa marehemu Regia, kwenye gari tayari kwa safari.
 

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Ubungo kupitia Chama hicho, John Mnyika, wakiangalia kwa huzuni.

Mbowe na Mnyika wakiwa na huzuni, wakati jeneza lenye mwili wa marehemu Regia ukiingizwa kwenye gari, tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda kwao Morogoro kwa mazishi.
 

Wafuasi wa Chadema, wakiwaaga wenzao waliokuwa wakisafiri kwenda kwenye mazishi Morogoro, huku wakionesha alama ya vidole viwili, inayotumiwa na chama hicho.


Baadhi ya wanachama wa Chama hicho, wanaosafiri na mwili wa marehemu Regia Mtema kwenda Morogoro kwa mazishi nao wakipunga na kuonesha ishara ya vidole viwili inayotumiwa na Chama hicho.


Sehemu ya umati wa wananchi waliojitokeza viwanja vya Karimjee, ukisubiri kuaga mwili huo. 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa (kulia) ,akimfariji pacha wa marehemu Regia katika hafla hiyo.

Mama mdogo wa marehemu Regia Mtema, Benadeta Mtema (wa pili kushoto), akilia kwa uchungu. Mama huyo ni mmoja wa watu waliojeruhiwa katika ajali iliyomuua Regia. Kulia ni Baba mzazi wa Regia. Estalatus Mtema.

Msafara ukiongozwa na askari wa Usalama Barabarani, ukiondoka Karimjee kuelekea Ifakara, Morogoro kwa mazishi.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara, Morogoro kwa mazishi.

Spika mstaafu Samuel Sitta, akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Regia.
 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambaye pia ni Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (katikati) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Uratibu na Bunge), William Lukuvi, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu, Regia Mtema.


Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema na Bob Makani wakitoa heshima za mwisho.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na Mbunge wa Bumbuli, Januari Makamba wakitoa heshima za mwisho.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, akimfariji pacha wa marehemu Regia Mtema.
 

Waombolezaji wakiendelea kutoa heshima za kuuaga mwili wa marehemu Regia Mtema.

Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi (kushoto), akimfariji Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.



Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro, Suzan Kiwanga (CHADEMA), akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto.





Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi (kulia), akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa CHADEMA, ambaye pia ni Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe (wa pili kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (wa pili kushoto) na Profesa Mwesiga Baregu wa CHADEMA.


Vijana wa Mtandao wa Jamii Forum, wakiwa wamevalia rasmi fulana za mtandao huo, waliposhiriki kuuaga mwaili wa aliyekuwa mwanachama wa mtandao huo, marehemu, Regia Mtema.


No comments:

Post a Comment