TANGAZO


Tuesday, January 17, 2012

Tanzania, Japan zasaini msaada wa Kilimo cha Umwagiliaji

 Kaimu Mkurugenzi, Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda  na Burundi kwa Kanda ya Afrika, ambaye ni mratibu wa mradi wa Kilimo cha umwagiliaji nchini, Mercy Tembon, akizungumza wakati wa utiaji wa saini makubaliano kati ya Tanzania na Japan, msaada wa kuiwezesha Tanzania katika mradi huo, leo asubuhi.


 Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijja, akizungumza wakati wa kutia saini na Japan makubaliano ya msaada wa kuiwezesha Tanzania katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji, Dar es Salaam leo asubuhi wizarani hapo. Kulia ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada na katikati ni Kaimu Mkurugenzi, Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda  na Burundi kwa Kanda ya Afrika, ambaye ni mratibu wa mradi huo, Mercy Tembon. (Picha na Kassim Mbarouk)



Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ramadhan Khijja (kushoto), akimshukuru Balozi wa Japan nchini Tanzania, Masaki Okada, mara baada ya kutia saini makubaliano ya msaada wa kuiwezesha Tanzania katika mradi wa Kilimo cha Umwagiliaji, Dar es Salaam leo asubuhi wizarani hapo. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi, Mkazi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi kwa Kanda ya Afrika, ambaye ni mratibu wa mradi huo, Mercy Tembon.

No comments:

Post a Comment