Makamu aa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal na mkewe
Mama Zakhia Bilal, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu. Mwili wa marehemu Regia umeagwa leo Januari 17, katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwao Ifakara kwa mazishi. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal (kulia), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa pili kushoto), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Anne Makinda (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, leo katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakhia Bilal, wakiagana na wanafamilia ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari.
Mke wa Makamu wa Rais, Mama Zakhia Bilal, mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda, Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, wakiwa katika shughulia ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, marehemu Regia Mtema, Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Mama Tunu Pinda, wakitoa heshima za mwisho kwa mwili
wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyefariki
mwishoni mwa wiki kwa ajali ya gari eneo la Daraja la Mto Ruvu.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, Anne Makinda na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakiwa katika shughulia ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia CHADEMA, marehemu Regia Mtema, aliyeagwa leo katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Regia anatarajia kuzikwa kesho nyumbani kwao Ifakara.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akitoa salama za rambirambi kwa niaba ya Serikali.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, akitoa wasifu wa marehemu Regia Mtema katika shughuli za Kibunge na salam za rambirambi kwa niaba ya Bunge.
Makamu wa Rais wa Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Tundu Lissu, Vita Kawawa, pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia, wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee, leo.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na kuagana na Andrew Chenge pamoja na baadhi ya wananchi waliohudhuria shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu Regia, wakati akiondoka katika viwanja hivyo vya Karimjee leo.
No comments:
Post a Comment