Mmoja wa waathirika wa mafuriko, Lucy Asheri, akiingia kwenye moja ya mahema yaliyojengwa na Serikali kwa ajili ya makazi yao ya muda, leo mchana, wakati walipotembelea kijiji cha Mabwepande, kuangalia maendeleo ya ujenzi huo pamoja na upimaji wa viwanja vyao. (Picha na Kassim Mbarouk)
Baadhi ya waathirika wa mafuriko kutoka iliyokuwa kambi ya Hananasif, kutoka kushoto, Adinan Mnyachi, Lucy Asheri na Devota Pango, wakiwa mbele ya moja ya mahema yaliyojengwa kwa ajili yao, walipofika kwenye mradi wa ujenzi wa makazi ya muda watakayohamishiwa, kuangalia maendeleo yake leo mchana. Kulia ni Maofisa wa Red Cross, wanaoshughulika na mradi huo.
Waathirika hao, wakisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, wakati walipofika kwenye kijiji cha Mabwepande, watakakohamishiwa na Serikali.
No comments:
Post a Comment