Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Gabriel Fuime, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati alipouwa akizungumza nao kwenye mradi wa makazi mapya ya waathirika wa mafuriko, Mabwepande Kinondoni, Dar es Salaam, leo mchana. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati walipotembelea mradi wa kuwahamishia waathirika wa mafuriko, kijiji cha Mabwepande, leo mchana kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mahema kwa ajili ya makazi ya muda na upimaji wa viwanja kwa ajili ya waathirika hao.
Gari la kubebea maji safi likijaza matenki ya kuhifadhia maji kwenye kijiji cha Mabwepande, watachohamishiwa waathirika wa mafuriko. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mmoja wa kijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), akifanya usafi kwenye sehemu ya kujenga hema kwa ajili ya waathirika hao.
Vijana wa Jeshi la Kujega Taifa (JKT), wakifunga hema kwenye miti waliyoisimika.
Vijana wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), wakijenga miti kwa ajili ya kufunga hema kwa ajili ya waathirika hao, kijijini hapo leo mchana.
No comments:
Post a Comment