TANGAZO


Monday, January 9, 2012

Diamond ahukumiwa miezi 6 kwa kumfanyia vurugu mwandishi





Msanii Diamond na mcheza show wake wakiwa nje ya Mahakama ya Mwanzo, mjini  Iringa

Mdhamini wa msanii Diamond, Edo Bashir (kushoto), akizungumza na mmiliki wa mtandao Francis Godwin, ambaye ndiye mlalamikaji katika kesi hiyo.

Msanii wa muziki wa Kizazi kipya, Diamond amewasili mjini Iringa na atapandishwa Mahakama ya Mwanzo, Bomani asubuhi hii. (Picha na Francis Godwin)



Mkapa akiwasili nyumbani kutoka Afrika Kusini 

 

Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akilakiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama alipowasili leo Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, akitoka Afrika Kusini ambako alimwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika maadhimisho ya miaka 100 ya chama cha ANC. Kati niu Mama Anna Mkapa.

 



Polisi Mbeya wapata Mkuu mpya wa Upelelezi
Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi (RCO), Mkoa wa Mbeya, Chacha (wa pili kulia), akiwa na mtunza hazina wa MUJATA, mkoani Mbeya, Kanali Mstaafu, Silvester Matiko (wa kwanza kulia), akikaribishwa katika Ukumbi wa mji mdogo wa Mbalizi katika sherehe za kumuaga aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi hilo mkoani (RCO), Anacletus Malindisa anayehamia Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es salaam.

Kutoka kushoto, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya (RCO), Anacletus Malindisa, anayehamia Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es salaam,  Mwenyekiti wa MUJATA mkoani hapa, Chifu Shayo Soja wakati wa sherehe za kumuaga na kumkaribisha RCO mpya. (Picha na Ezekiel Kamanga)

Magari matatu yangongana jioni hii, mjini Mbeya

Magari matatu yamegongana jioni hii, maeneo ya Mwanjelwa, dereva wa gari aina ya Toyota Carina alisimama ghafa na ndipo magari yaliyofuatia nyuma yake, yakashindwa kushika breki na kugongana.



Moja ya magari hayo, yakiwa yameligonga gari aina ya Toyota Hice kwa nyuma.


Gari aina ya Toyota Carina, likiwa limegongwa kwa nyuma na Toyota Hice, baada ya nalo kugongwa na mwenzake kwa nyuma katika ajali hiyo.


Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (katikati), akiwa katika picha na wapigapicha wa vyombo mbalimbali vya habari, Dar es Salaam, leo baada ya hafla ya kusaini mkataba wa ujenzi wa daraja jipya la Kigamboni. (Picha na Mdau wetu)

Mkataba wa Ujenzi wa daraja la kigamboni watiwa saini 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dk. Ramadhan Dau (kushoto), akibadilishana hati za makubaliano ya ujenzi wa daraja la Kigamboni na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ujenzi ya  China Railway Engineering Group Co. Limited, Shi Yuan baada ya kutiliana saini mkataba wa ujenzi huo leo asubuhi, Dar es Salaam . Wanaoshuhudia ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli (wa pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick (katikati) na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka. (Picha na Richard Mwaikenda)

Dk. Dau akisaini mkataba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni itakayojenga daraja la Kigamboni, Dar es Salaam, Shi Yuan.

Wakibadilishana hati za mkataba huo

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa hafla hiyo.

Wakiwa katika picha ya pamoja baada kusaini mkataba huo.

 Dk. Dau akipongezwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick.

 Waziri wa Ujenzi akijadiliana jambo na Mtangazaji wa Radio Clouds, Ephraem Kibonde aliyekuwa MC wa hafla hiyo.

         Wapigapicha wakifurahi pamoja na Waziri wa Ujenzi, Dk. Magufuli, mara baada ya kusainiwa kwa mkataba wa ujenzi wa daraja la Kigamboni.

No comments:

Post a Comment