TANGAZO


Monday, January 9, 2012

Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa, yatembelea Mabwepande


Mhandisi wa mradi wa Mabwepande kwa ajili ya kuwahamishia waathirika wa mafuriko, Ismail Mafita, akiwaelezea baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, waliotembelea kwenye mradi huo, leo mchana, kuhusu namna walivyovipima viwanja vya waathirika hao, kijijini hapo. (Picha na Kassim Mbarouk)



 Mhandisi wa mradi wa Mabwepande kwa ajili ya kuwahamishia waathirika wa mafuriko, Ismail Mafita, akiwaongoza wajumbe hao kutembelea mahema na viwanja vilivyopimwa kwa ajili ya waathirika hao.





 Mratibu wa Ujenzi wa mahema ya waathirika wa mafuriko, Aidan David wa Red Cross, akiwapatia maelezo wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkowa wa Dar es Salaam, wakati wa ziara yao hiyo, kuhusu uimara wa mahema hayo pamoja na hatua waliyofikia hadi sasa.




 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ramadhan Madabida, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wajumbe wa Kamati hiyo, walipomaliza ziara yao ya kutembelea, kijiji cha Mabwepande watakachohamia waathirika wa mafuriko.





 Mhandisi wa mradi wa Mabwepande kwa ajili ya kuwahamishia waathirika wa mafuriko, Ismail Mafita (katikati), akiwaongoza wajumbe wa Kamati hiyo, kuangalia moja ya mahema waliyoyajenga katika mradi huo, leo mchana. Kushoto ni mjumbe Zarina Madabida, Mbunge wa Viti Maalum na kulia ni Juma Simba, Katibu wa Siasa na Uenezi.

No comments:

Post a Comment