Shirika la kimataifa la misaada
ya matibabu, MSF, limeanza kuwatibu wagonjwa katika mji wa Pibor, Sudan
Kusini, ambako kulitokea mapigano ya kikabali yaliyouwa mamia ya watu.
Mkuu wa MSF Sudan Kusini, Parthesarathy Rajendran, aliiambia BBC kwamba wenyeji wa eneo hilo, kabila la Murle, wameanza kurudi katika mji huo, kwenye jimbo la Jonglei, ambao ulihamwa wakati wa mapigano na kabila la Lou Nuer.
Alisema MSF sasa imewasiliana na wafanyakazi wake wote waliokimbilia vichakani wakati wa mapigano, lakini 47 bado wametoweka.
No comments:
Post a Comment