Ofisa Mkuu wa Masoko na
Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba (kushoto), akipokea zawadi ya mbuzi
toka kwa baadhi ya wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Ruvu Darajani,
iliyopo mkoani Pwani, mara baada ya kuwakabidhi rasmi vyumba vitatu vya madarasa
na madawati 100 kwa ajili ya shule hiyo. Msaada huo uliotolewa na Vodacom
Foundation na umegharimu zaidi ya shilingi Milioni 98.
Madarasa mapya yaliyokabidhiwa kwa shule ya
msingi ya Ruvu Darajani na Vodacom Foundation, iliyopo Mkoani Pwani jana.
Mkurugenzi wa Wizara ya Elimu
kwa shule za Msingi, Zuberi Samataba, mwenye suti akiongea jambo na 0fisa Mkuu wa
Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania, Mwamvita Makamba,walipowasili katika
shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani Pwani kwa ajili ya kukabidhi
msaada wa madarasa matatu na madawati 100, yaliyotolewa na Vodacom Foundation
katika shule hiyo na kugharimu zaidi ya shilingi Milioni 98.
Hili ndilo jiko la wanafunzi wa
Shule ya Msingi ya Ruvu Darajani, iliyopo mkoani Pwani.
Kikundi cha ngoma cha wazazi wa
mkoa wa Pwani , kikitumbuiza wakati wa makabidhiano ya vyumba vitatu vya
madarasa pamoja na madawati 100, vilivyokabidhiwa na
Vodacom Foundation kwa ajili ya shule ya msingi ya Ruvu Darajani, mkoani
Pwani. Msaada huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 98.
0fisa Mkuu wa Masoko na
Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba, akikata utepe kuashiria uzinduzi
wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja na madawati 100 vilivyokabidhiwa na
Vodacom Foundation kwa ajili ya shule ya msingi ya Ruvu Darajani iliyopo Mkoani
Pwani.
No comments:
Post a Comment