Baadhi ya wahadhiri wa Taasisi hiyo, wakiingia kwenye viwanja hivyo, tayari kwa mahafali hayo ya Tano ya DIT leo.
Baadhi ya wageni waalikwa kutoka taasisi mbalimbali jijini, wakiingia kwenye viwanja vya mahafali hayo, nyuma ya mgeni rasmi, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, aliyeingia mwanzo viwanjani humo.
Mgeni Rasmi, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa (katikati), akiwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga (kushoto) na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Fredrick Mwanuzi, wakiimba wimbo wa Taifa katika mahafali hayo.
Mgeni Rasmi, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa (katikati), akiwatunuku wahitimu wa Stashahada ya Civil Engineering, katika mahafali hayo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga na kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Fredrick Mwanuzi.
Mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi kuwazidi wenzake, Michael Christopher, akimpa mkono mgeni katika mahafali hayo, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa,
Mgeni rasmi wa mahafali hayo, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa (katikati), akipigapicha ya pamoja na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye masomo yao, wakati wa mahafali hayo.
Mgeni rasmi wa mahafali hayo, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, akisindikizwa na Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Fredrick Mwanuzi (kulia anayezungumza naye) na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Charles Kitwanga (kushoto), wakati akiondoka kwenye viwanja vya mahafali vya DIT, mara baada ya kuyafunga rasmi mahafali ya Tano ya DIT, leo mchana. (Picha na Kassim Mbarouk)










No comments:
Post a Comment