TANGAZO


Saturday, January 28, 2012

Mahafali ya 5 ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)

 Bango la mahafali ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), lililokuwa limewekwa kwenye viwanja vya michezo vya DIT, yalikofanyika mahafali, likielezea kuhusu mahafali hayo. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Kikosi cha Jeshi la Polisi (Police Brass Band), kikiongoza maandamano ya wahitimu wa Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT), wakati wa mahafali yao hayo, leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Wahitimu wa Shahada mbalimbali wa Taasisi hiyo, wakiwa kwenye maandamano ya kuingia kwenye viwanja vya mahafali, katika viwanja vya michezo vya DIT.


 Baadhi ya wahitimu wa Taasisi hiyo, wakiwa wamekaa tayari kwa ajili ya kutunukiwa shahada mbalimbali katika mahafali yao ya Tano ya DIT, leo jijini.


 Kikundi cha ngoma cha Jeshi la Polisi, kikitumbuiza kabla ya mgeni rasmi, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, kuwasili kwenye viwanja vya mahafali hayo ya DIT.


 Wasanii wakike wa kundi hilo, wakicheza ngoma ya asili ya Singoda kwenye mahafali hayo.


Wasanii wakinengua kwa pamoja ngoma hiyo ya wenyeji wa Singida, iitwayo Mgodo.

No comments:

Post a Comment