TANGAZO


Sunday, January 29, 2012

Serengeti yazindua nembo mpya ya dhahabu lakini ladha ile ile

Kutoka kulia ni Emilian Rwejuna, Meneja Masoko (SBL), Mark Tyro, Mkurugenzi wa Usambazaji, Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko, Mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko. Joyce Mapunjo, Mkurugenzi Mtendaji wa (SBL), Richard Wells na kushoto ni Zohra Moore, Meneja wa Huduma IPP wakipozi kwa picha huku wakiwa wameshikilia chupa mpya ya Serengeti Lager iliyo katika muonekano wa Dhahabu.
 
 
Chupa mpya ya Serengeti Lager yenye muonekano wa wa Dhahabu ikiibuka kutoka katika maji mara baada ya kuzinduliwa rasmi jana usiku.
 
 
Shamrashamra zikiendelea wakati nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager ikizinduliwa jana.
 
 
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda Biashara na Masoko B. Joyce Mapunjo akizungumza katika uzinduzi huo
 
 
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells akizungumza katika uzinduzi huo wakati alipomkaribisha mgeni rasmi.
 
 
Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti akizungumzia mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika taifa kupitia bia ya Serengeti Lager.
 
 
 
Mark Tyror Mkurugenzi wa Usambazaji kulia na Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti wakionyesha nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager.
 
 
Mrembo wa Serengeti Lager akipozi kwa picha na huku akionyesha Nembo mpya ya bia ya Serengeti Lager. 
 
 
Mkurugenzi wa Usambazaji Mark Tyro kushoto akipozi kwa picha na marafiki zake.
 
 Kutoka kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Richard Wells, Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti na Mwisho ni Meneja wa Mahusiano kampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela.
 
 
Hapa ilibaki burudani tu.
 
 
 
Ephraima Mafuru Mkurugenzi wa Masoko kampuni ya bia ya Serengeti akiongea na mkurugenzi wa Extra Bongo Kamalade Ali Choki , kulia ni Meneja Masoko wa (SBL) Emilian Rwejuna.
 
 
Hapa mzuka ukapanda kidogo lakini yote ilikuwa burudani na uzinduzi wa muonekano wa Dhahabu katika burudani ileile ya Serengeti Lager.
 
 
Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.
 
 
Kikundi cha ngoma za asili kikitoa burudani katika uzinduzi huo.
 
 
Dada Ritah Mchaki Meneja wa bia ya Tusker (katikati), akipozi na wadau kutoka kampuni ya bia ya Serengeti . (Picha na Mpigapicha  wetu)

No comments:

Post a Comment