Mmoja wa makocha wa Simba akiwaelekeza wachezaji namna ya kufanya kwenye mazoezi ya timu hiyo, Uwanja wa Sigara, Dar es Salaam, leo jioni.
Wachezaji wa timu y Simba wakikimbia huku wakiruka juu ili kujiweka sawa kimwili na kiakili kabla ya kucheza raundi ya Pili ya michuano ya Ligi Kuu ya Vodaom, mwishoni mwa mwezi huu.
Mwalimu wa makipa, golikipa wa zamani wa timu ya Simba, James Kisaka, akiwa na mipira yake kwa ajili ya zoezi la kuwanoa magolikipa wa timu hiyo, Uwanja wa Sigara, Chang'ombe, Dar es Salaam jana.
Mchezaji Dereck Waluliya (kushoto), akipambana na Gervais Kago wote wa Simba wakati wa mazoezi ya timu hiyo, kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Sigara, Dar es Salaam jana. (Picha na Kassim Mbarouk)
Waluliya (kulia), akipambana na Machaku Salum (kushoto) katika mazoezi hayo, leo jioni.
No comments:
Post a Comment