Wednesday, January 18, 2012
Shirika la Posta laadhimisha Siku ya Posta Afrika, lasaidia waathirika wa mafuriko
Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Deos Mndeme (kushoto), akimkabidhi moja ya ndoo za mafuta ya kula, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, ikiwa ni sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali, vikiwemo vyakula, sabuni, nguo na magodoro kwa ajili ya waathirika wa mafuriko, ikiwa ni sehemu ya madhimisho ya Siku ya Posta Barani Afrika yaliyoadhimishwa jijini leo. Msaada huo, ulikuwa na thamani ya sh. milioni 5.2. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, akimshukuru Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Deos Mndeme (kushoto), baada ya kukabidhi msaada huo, leo asubuhi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, akizunguma katika hafla hiyo, ambapo alilishukuru Shirika la Posta Tanzania, kwa msaada huo na kuwashauri kuweka kitu ambacho kitawaletea kumbukumbu katika maadhimisho hayo kwa waathirika hao, hasa ifikapo wakati kama huu, wa maadhimisho, waweze kwenda kukitembelea. Kushoto ni Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Deos Mndeme. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, waliofika katika hafla hiyo. Kushoto ni Posta Masta Mkuu wa Shirika hilo, Deos Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki, akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania, akiwa na Posta Masta Mkuu, Deos Khamisi Mndeme (wa pili). Kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano na Masuala ya Kimataifa, Elia Madulesi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki (katikati), akiwa na Posta Masta Mkuu, Deos Mndeme (kulia kwake) na baadhi ya wafanyakazi wa Shirika hilo, katika picha ya pamoja, waliohudhuria katika hafla hiyo, Ofisini kwa Mkuu huyo wa Mkoa, leo asubuhi.
Posta Masta Mkuu, Deos Mndeme, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment