Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazi kama ishara ya kuzindua picha ya kuchora kwa penseli, iliyochorwa na msanii Haji Simba (wa pili kushoto), wa kikundi cha Zan Artist cha Hurumzi, mjini Zanzibar. Picha hiyo, iliyofanana kabisa na sura yake, ambayo inaonesha anachuma karafuu, imechorwa kwa muda wa miezi miwili, sawa na siku 60, hadi kumalizika kwake. Wa tatu kulia ni Mshauri wa Rais, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Abrahmani Mwinyi Jumbe na wapili kulia ni Mkurugenzi wa Kamisheni ya Utalii, Ali Khalil Mirza. (Picha na Ramadhan Othman Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiiangalia picha iliyochorwa na msanii, Haji Simba (kushoto), wakati alipoizindua picha yake hiyo ya kuchorwa leo mjini Zanzibar. (Picha na Ramadhan Othman Ikulu)
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipata maelezo kutoka kwa msanii wa uchoraji, Haji Simba, aliyechora picha yake, akiwa anachuma karafuu, wakati alipozindua uchumaji wa zao la karafuu kisiwani Pemba.
No comments:
Post a Comment