Baadhi ya ndugu wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, marehemu Regia Mtema (Chadema), wakilia wakati mwili ulipowasili Ifakara, Morogoro jana alfajiri. (Picha na Mdau wetu)
Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), marehemu Regia Mtema, ukiwasili nyumbani kwao, Ifakara, Morogoro leo alfajiri kutoka Dar es Salaam kwa ajili ya mazishi.
Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, akibeba shada la maua kwenda kuliweka kwenye kaburi la marehemu Regia Mtema, mara baada ya mazishi nyumbani kwao, Ifakar, Morogoro leo. (Picha na Ikulu)
Rais Jakaya Kikwete, akiweka shada la mau kwenye kaburi la marehemu Regia Mtema.
Rais Jakaya Kikwete, akiweka, akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Regia Mtema kwenye mazishi hayo, leo mjini Ifakara, Morogoro.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda (kushoto kwake), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia kwake), baadhi ya viongozi wa Chadema pamoja na waombolezaji kwenye shughuli za mazishi, Ifakara, nyumbani kwao marehemu Regia Mtema.
Rais Jakaya Kikwete, akiwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda (kushoto kwake), Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia kwake), Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe (kushoto) pamoja na waombolezaji wengine, kwenye shughuli za mazishi hayo.
No comments:
Post a Comment