TANGAZO


Tuesday, January 31, 2012

Benki ya Posta yangia mkataba wa ukusanyaji mapato na TRA


Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kushoto), akifafanua jambo kwenye mkutano na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati alipokuwa akielezea kuhusu mkataba kati ya benki hiyo na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambapo matawi yote ya benki hiyo, yatapokea malipo ya kodi ya mapato na malipo ya leseni za udereva. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Elimu kwa mlipakodi wa TRA, Allan Kiula. Mkutano huo, umefanyika leo, Makao Makuu ya benki hiyo jijini. (Picha na Noves Moses wa TPB)



Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kushoto), akishikana mkono na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu kwa mlipa kodi wa TRA, Allan Kiula, wakati walipokuwa wakikabidhiana mkataba huo, mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani), Dar es Salaam leo. Mkataba ambao benki hiyo matawi yake yote, yatapokea malipo ya kodi ya mapato na malipo ya leseni za udereva.


 Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Sabasaba Moshingi (kushoto), akizungumza jambo, mara baada ya kukabidhiana mkataba na Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Allan Kiula (kulia), kuhusu benki ya Posta, kukusanya kodi ya mapato na leseni za udereva.

No comments:

Post a Comment