Mwendesha pikipiki akiwa ameanguka chini kwenye barabara ya Kawawa, maeneo ya Ilala Boma, baada ya pikipiki yake kuteleza na kumdondosha chini, barabarani huku kofia ya kumkinga na ajali (helmet), ikiwa imevuka kichwani, hatua iliyomsababishia kuumia sehemu ya paji lake la uso, leo asubuhi. (Picha na Kassim Mbarouk)
Wananchi wakijaribu kumsaidia kwa kumtafutia gari la kumpeleka hospitali kwa ajili ya kupatiwa huduma ya matibabu.
Mwendesha pikipiki akiwa amelala bila kujitambua, huku wananchi wakitaka kumatia msaada, baada ya kupata ajali ya kudondoka kwenye pikipiki yake wakati akiwa kwenye barabara ya Kawawa, maeneo ya Ilala Boma, Dar es Salaam.
Wasamaria wema, wakimbeba kwa ajili ya kumwingiza kwenye gari la kumpeleka hospitali, kijana mwendesha pikipiki, aliyedondoka na kuumia sehemu ya paji lake la uso, kutokana na kuteleza kwa pikipiki hiyo, wakati akiiendesha maeneo ya Ilala Boma, barabara ya Kawawa, Dar es Salaam leo. (Picha na Kassim Mbarouk)





No comments:
Post a Comment