TANGAZO


Tuesday, January 31, 2012

Mfuko wa Sanaa Tanzania (TASAFO), wazinduliwa

 Msemaji wa Mfuko wa Sanaa Tanzania (TASAFO), Ramadhan Kanzaga, akizungumza na waandishi wa habari, ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo Dar es Salaamm leo, wakati wa uzinduzi wa Mfuko wa huo. Kulia ni Ofisa Sanaa Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Malimi Mashili, aliyekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo, akimwakilisha Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Gonche Materego. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Ofisa Sanaa Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Malimi Mashili, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo wakati wa alipokuwa akiuzindua Mfuko wa Sanaa Tanzania (TASAFO), Idara ya Habari, Maelezo. Kushoto ni Katibu wa Bodi ya TASAFO, Shekha Said na katikati ni Msemaji wa mfuko huo, Ramadhan Kanzaga.


 Msemaji wa Mfuko wa Sanaa Tanzania (TASAFO), Ramadhan Kanzaga (kushoto), akimkabidhi cheti cha Uzinduzi wa mfuko huo, Ofisa Sanaa Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Malimi Mashili kwa ajili ya kukisaini, wakati wa uzinduzi wa mfuko huo, Dar es Salaam leo. Katikati ni Katibu wa Bodi ya TASAFO, Shekha Said.



 Baadhi ya waandishi wa habari, wakishuhudia uzinduzi wa Mfuko huo, ukumbi wa Idara ya Habari, Maelezo, Dar es Salaam leo.


Baadhi ya waandishi wa habari, wakifuatilia maelezo mbalimbali ya uzinduzi yaliyokuwa yakitolewa na mgeni rasmi katika uzinduzi huo, Ofisa Sanaa Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Malimi Mashili. 

No comments:

Post a Comment