TANGAZO


Tuesday, January 31, 2012

Airtel yaendesha Semina ya kuelimisha wateja, makampuni na kuzindua Airtel money

 Mkurungezi wa fedha wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Kalpesh Mehta, akitoa semina ya huduma ya Airtel money kwa mashirika na wadau mbalimbali walioalikwa na kuhudhuria semina hiyo, iliyofanyika leo na kuendeshwa kwa siku mbili Makao  Makuu ya Airtel , lengo likiwa ni kuwaeleimisha wafanyabiashara na mashirika mbalimbali jinsi huduma ya Airtel money inavyoweza kutoa suluhisho la matatizo yanayowapata katika kuendesha biashara zao.



 Mkurungenzi wa Kampuni ya simu za mkononi  ya Airtel, Sam Elangallor (kulia), akionesha kwa vitendo jinsi gani huduma ya Airtel money inavyofanya kazi na kutoa shuluhisho kwa changamoto wanazozipata katika kuendesha biashara kwa wawakilishi kutoka katika makapuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo. iliyofanyika Makao makuu ya Airtel. Anayefata ni Mkurungezi wa Fedha, Kalpesh Mehta na Meneja Huduma Airtel money, Asumpya Naligingwa.



 Mkurungenzi wa Kampuni ya Airtel, Sam Elangallor, akitoa semina ya huduma ya Airtel money  kwa wawakilishi kutoka katika Makampuni mbalimbali waliohudhuria semina hiyo.



 Mkurugenzi wa Mahusiano wa Airtel, Beatrice Singano, akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa semina ya Airtel money, inayotolewa kwa Makapuni mbalimbali kwa muda wa siku mbili.
Mmoja wa wakilishi kutoka katika Makampuni yaliyohudhuria semina ya huduma za Airtel money akichangia hoja wakati wa semina hiyo, iliyozinduliwa rasmi leo na kuendeshwa na Mkurugenzi wa Airtel, Sam Ellangallor na Mkurugenzi wa fedha, Kalpesh Meltha katika ofisi za Makao Makuu ya Airtel.

No comments:

Post a Comment