TANGAZO


Thursday, January 19, 2012

Mahakama Kuu yaanza kusikiliza kesi iliyofunguliwa na Hamad Rashid

 

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro akiwa na baadhi ya wanachama wa Chama hicho, wakitoka Mahakama Kuu, kusikiliza kesi iliyofunguliwa na baadhi ya wanachama waliofukuzwa uanachama na Baraza Kuu la Uongozi, wakiongozwa na Mbunge wa Wawi, kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohamed, wakidai warejeshewe uanachama wao kwa kuwa wamefukuzwa isivyo halali na Baraza hilo na pia kukiukwa amri ya mahakama ya kulitaka baraza hilo, kutowajadili wala kuwafukuza unachama. (Picha na Kassim Mbarouk)


Mbunge wa Wawi kisiwani Pemba, Hamad Rashid Mohamed, akitoka katika Mahakama Kuu, Dar es Salaam, baada ya kuahirishwa kwa maombi ya kutaka kujua hatima ya zuio la mahakama lililopuuzwa na viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF), katika kikao cha kuwafukuza uanachama. Kulia ni aliyekuwa Mbunge wa Micheweni, kisiwani humo, Shoka Khamis Juma na kushoto ni aliyekuwa mgombea wa chama hicho, Jimbo la Segerea, Kimangale Mussa. (Picha na Kassim Mbarouk)

No comments:

Post a Comment