Cisse, ambaye ameshapachika mabao 15 katika mechi za ligi msimu huu, atavaa fulana namba tisa katika klabu ya Newcastle.
"Ni heshima kuichezea klabu kubwa kama hii," alisema baada ya kumwaga wino.
Cisse atafuata nyayo za wachezaji maarufu waliowahi kuvaa fulana yenye namba tisa katika klabu ya Newcastle, akiwemo Hughie Gallacher, Jackie Milburn, Wyn Davies, Malcolm MacDonald, Mick Quinn, Andy Cole, Les Ferdinand na Alan Shearer ambao walikuwa mashuhuri kwa kupachika mabao katika klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa Senegal, ambaye ameshapachika mabao saba katika mechi 12 za kimataifa, alifunga bao moja wakati Senegal walipoilaza Kenya wakijiandaa kwa Kombe la Mataifa ya Afrika, michuano itakayoanza siku ya Jumamosi huko Equatorial Guinea na Gabon.
"Ningependa kumshukuru kila mmoja kwa kunikaribisha na kunialika nijisajili katika klabu hii," aliongeza Papiss.
"Nitajitahidi kulipa fadhila kutokana na imani ambayo klabu imenionesha na nitawapatia mashabiki kile roho inapenda.
"Ninafahamu umuhimu wa kuvaa fulana yenye namba tisa na nilipozungumza na meneja, aliweka wazi umuhimu wa fulana hiyo."
"Nitaiheshimu na natumai kufanya kila niwezalo kwa heshima ya fulana hii."
Ingawa Cisse msimu huu thamani yake ilikuwa kama paundi milioni 14, inaaminika Newcastle imelipa fedha zinazokaribia paundi milioni 10 kwa ajili ya kumpata mrithi huyo wa Andy Carroll, aliyejiunga na Liverpool kwa kitita kinachofikia paundi milioni 35 katika dirisha dogo la usajili la mwezi wa Januari mwaka 2011.
Meneja wa Newcastle Alan Pardew amekiri: "Tangu alipoondoka Andy Carroll, Papiss alikuwa chaguo langu la kwanza katika nafasi hiyo muhimu ya ushambuliaji."
Mkurugenzi mtendaji wa Newcastle Derek Llambias ameongeza: "Tunafuraha kubwa tumempata Papiss.
No comments:
Post a Comment