TANGAZO


Monday, January 30, 2012

Cheka alivyomchakaza Nyilawila, Uwanja wa Jumhuri Morogoro

  Bondia Ibrahimu Class (kushoto), akipambana na Venasi Mponji katika pambano la utangulizi kabla ya Francis Cheka kutwangana na Karama Nyilawila, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro juzi usiku. (Picha na Rajab Mhamilwa Super D, Mnyamwezi) 


Bondia Ibrahimu Class (kushoto), akimtupia konde la kushoto Venasi Mponji katika pambano hilo, uwanjani hapo.


Bondia Francis Cheka (kulia), akimtupia konde la mkono wa kushoto, Karama Nyilawila, wakati wa mpambano wao huo, uwanjani hapo.

Karama Nyilawila (kushoto), akikwepa konde la mkono wa kushoto la Francis Cheka, katika mpambano huo ulioishia kwa Cheka kushinda kwa pointi.



Bondia Karama Nyilawila (kulia), akipenyeza ngumi ya mkono wa kushoto, kidevuni mwa Francis Cheka katika pambano hilo.


Cheka akitangazwa kushinda kwa pointi na mwamuzi wa mpambano huo. Kushoto ni Karama Nyilawila.


Cheka akinyanyua mikono juu kuashiria ushindi dhidi ya mpinzani wake huyo, Karama Nyilawila.


Askari Polisi wakiwatuliza mashabiki wakati wa mpambano huo, uliokuwa wa upinzani mkali.

No comments:

Post a Comment