TANGAZO


Saturday, January 28, 2012

Bosi wa TBS, aonjeshwa joto ya jiwe na Kamati ya Bunge kwa madai ya Utapeli


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Charles Ekelege, akiwa hoi, wakati Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Deo Filikunjombe (hayupo pichani), akimshutumu kwa utendaji wake mbovu, uliojaa utapeli ambao Kamati hiyo, iliugundua katika ziara zake nje ya nchi, kukagua kampuni za ukaguzi wa magari yanayoingizwa nchini. Filikunjombe alikuwa anazungumza hayo katika kikao cha kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (POAC) na PAC cha kujadili utendaji wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dar es Salaam jana. (Picha na Richard Mwaikenda)

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Deo Filikunjombe (kulia), akimshutumu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Charles Ekelege (picha ya juu) kwa utendaji wake mbovu, uliojaa utapeli, uliogunduliwa na kamati yake ilipokuwa katika ziara nje ya nchi. 

Ekelege akizungumza na waandishi wa habari, baada ya sakata hilo, hata hivyo hakutaka kufafanua jambo lolote , hivyo kuamua kuondoka na kuwaahidi kukutana nao leo, kuelezea kwa kina.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Esther Bulaya, akielezea jinsi alivyotapeliwa na wakala wa ukaguzi wa magari.

Mbunge Lugora, akielezea jinsi alivyo kasirishwa na ubabaishaji wa Ekelega na kuamua kumrushia ngumi ambayo ilidakwa na Mbunge Filikunjombe, wakiwa Ughaibuni baada kamati kupewa simu feki ya kampuni ya nje, inayokagua magari yanayoingizwa nchini.


Muonekano mwingine wa Ekelege wakati wa kikao hicho.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, Joyce Mapunjo (wa pili kulia), akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (PAC), Deo Filikunjombe (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (POAC), John Cheyo (kulia), baada ya kamati hizo, kumtajia uozo wa ukaguzi wa magari unaofanywa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), kwa kushirikiana na kampuni feki za nje ya nchi, leo wakati wa vikao vya Kamati za Bunge, Dar es Salaam. 

No comments:

Post a Comment