TANGAZO


Saturday, January 28, 2012

Bohari Kuu ya Madawa (MSD), yaisaidia Twiga Stars sh. mil. 10


Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo, akimkabidhi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah, mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 10, ikiwa ni msaada kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars, Dar es Salaam leo. Katikati ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia. Timu hiyo inacheza na Namibia kesho katika mchezo wa marudiano ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake. (Picha na Richard Mwaikenda)

Katibu Mkuu TFF, Angetile Osiah (kushoto), akitoa shukurani kwa MSD, kwa kuipatia timu hiyo msaada. Katikati ni Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo na kulia ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa gazeti la Jambo Leo, Grace Michael.

Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia, akielezea umuhimu wa msaada huo kwa timu hiyo ya soka ya wanawake. Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah.

No comments:

Post a Comment