Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu baada ya kumalizika kwa mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyofanyika jana katika kijiji cha Pahi kilichopo Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. Spika alikuwa Mgeni rasmi katika mashindasno hayo. wa pili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba, Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Mhe. Simon Odunga (kulia) na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaban (wa tatu kulia).(Picha zote na Ofisi ya BUNGE)Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu baada ya kumalizika kwa mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyofanyika jana katika kijiji cha Pahi kilichopo Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. Spika alikuwa Mgeni rasmi katika mashindano ya usomaji Quran yaliyofanyika jana kijijini hapo, kutoka kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba anaefuata ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaban. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu baada ya kumalizika kwa mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyofanyika jana katika kijiji cha Pahi kilichopo Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. Spika alikuwa Mgeni rasmi katika mashindano ya usomaji Quran yaliyofanyika jana kijijini hapo, kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaban. Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akimpatia zawadi kati ya washindi wa mashindano ya Quran yaliyofanyika jana katika Kijiji cha Pahi kilichopo Wilayani kondoa Jijini Dodoma. Kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaban, Spika alikuwa Mgeni rasmi katika mashindano ya usomaji Quran yaliyoandaliwa na Mbunge wa Viti Maluum kutoka Kondoa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji. Spika wa Bunge, Mhe, Job Ndugai (kushoto) akikabidhiwa mifuko mia tatu (300) ya simenti kutoka kwa Meneja wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Tawi la Dodoma, Ndg. Halima Makange katika tukio lililofanyika jana katika Kijiji cha Pahi kilichopo Wilayani Kondoa Jijini Dodoma. Mifuko hiyo imetolewa kwa ajili ya maendeleo ya elimu kijijini hapo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Shule na zahanati. Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba, wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu kijaji, Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia (kushoto), Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaban na Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Ndg. Simon Odunga aliemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma. Spika wa Bunge, Mhe. Job ndugai akizungumza na waumini wa dini ya kiislam na wakazi wa kijiji cha Pahi (hawapo kwenye picha) kilichopo Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma. Baada ya kufuturu futari iliyoandaliwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu kijaji. Wa pili kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba na kulia ni Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustafa Shaban.
Na Benny Mwaipaja, Kondoa
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka watanzania kuwa na uvumilivu wa masuala ya kidini ili nchi iendelee kuwa na amani, utulivu na maendeleo.
Ndugai ametoa wito huo katika Kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani Dodoma, alipokuwa akizungumza wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur'an yaliyowashirikisha zaidi ya watoto na vijana 40 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.
Spika Ndugai ameeleza kuwa umoja na mshikamano uliopo hapa nchini ni matokeo ya viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini kuendelea kuhubiri amani na utulivu na kuitaka jamii na viongozi hao kuiendeleza kazi hiyo.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameitaka jamii kuendelea kupiga vita uhalifu na kuwafichua wahalifu popote walipo ili nchi iendelee kuwa na amani.
Mratibu na Mwandaaji wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'an Tukufu ni kuwajengea vijana maadili mema ili waweze kushiriki kikamilifu kuleta maendeleo ya taifa.
Naye Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapher Shabaan amewapongeza vijana walioshiriki mashindano hayo na kuonesha umahili mkubwa wa kuhifadhi qoran na kuwataka waumini wa kiislamu kusoma na kukielewa kitabu hicho kitukufu kwa kuwa kimejaa elimu na maarifa mengi yatakayo wasaidia kuenenda vyema katika jamii na kupata thawabu kutoka kwa Mungu.
No comments:
Post a Comment