Takriba watu 22 wakiwemo watoto watatu wameuwa kwenye ajali ya basi kaskazini mwa Uganda kwa mujibu wa polisi.
Basi hilo liligonga tingatinga ambayo ikuwa ikiendeshwa bila ya taa usiku kwa mujibu wa msemaji wa polisi Emilian Kayima ambaye alingea na AFP.
Ajali hiyo ilitokea Ijumaa usiku huko Kiryandongo karibu kilomita 220 kaskazini mwa mji mkuu Kampala.
- Je unazifahamu nchi zinazotumia Kiswahili Afrika?
- Uganda yapinga ofisi za Umoja wa mataifa kuhamishwa Nairobi
- Maafisa wamsaka Chui aliyemla mtoto Uganda
Baadhi ya vyombo vya habari vilisema kuwa watu waliouawa walikuwa zaidi ya 30.
Uganda ina kati ya rekodi mbaya zaidi za usalama wa barabara. Zaidi ya watu 9,500 waliuawa kwennye ajali za barabarani nchini humo kati ya mwaka 2015 na 2017 kwa mujibu wa takwimu rasmi.


No comments:
Post a Comment