Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kulia) kuweka chupa ya kumwagilia kwa njia ya matone, hivi karibuni Wilayani Kishapu wakati wa kilele cha wiki ya upandaji miti nchini ambapo Kitaifa ilifanyika Mkoani Shinyanga.
Sehemu ya Msitu wa Hifadhi unajulikana kama Ngitili.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla (katikati) akishirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (kulia) kuweka fito za kuzuia wanyama,hivi karibuni Wilayani Kishapu wakati wa kilele cha wiki ya upandaji miti nchini ambapo Kitaifa ilifanyika Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa |Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiwahutubia wakazi wa Wilayani Kishapu hivi karibuni wakati wa kilele cha wiki ya upandaji miti iliyofanyika Kitaifa Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack (kulia) akiwahutubia wakazi wa Wilayani Kishapu hivi karibuni wakati wa kilele cha wiki ya upandaji miti iliyofanyika Kitaifa Mkoani Shinyanga. Kushoto ni Mkuu wa |Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri.
Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Kishapu wakichukua machapisho mbalimbali katika banda la Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya upandaji miti kitaifa iliyofanyika hivi karibuni mkoani Shinyanga.
Na Tiganya Vincent, RS Tabora
8 APRILI 2018
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku 30 kwa watu wote waliovamia hifadhi ya mistu maarufu kama “Ngitili” kuondoka haraka.
Hatua hiyo inalenga kukabiliana na uharibifu wa mazingira uliosababishwa na watu kuvamia misitu hiyo chini ya Mradi wa Hifadhi Aridhi Shinyanga (HASHI).
Waziri huyo alitoa kauli hiyo hivi karibuni, Wilayani Kishapu wakati wa kilele cha wiki ya upandaji miti nchini ambapo Kitaifa ilifanyika Mkoani Shinyanga.
Alisema Ngitili zilianzishwa kwa lengo la kurejesha uoto wa asili mkoani humo lakini baadhi ya watu wachache wasioitakia mema Shinyanga wameingia katika maeneo hayo na kujimilikisha huku kuendesha shughuli ambazo ni kinyume cha uhifadhi wake.
Dkt. Kigwangala alisema baada ya siku hizo kumalizika kama wahusika hawatakuwa wameondoka wenyewe kwa hiari itabidi nguvu itumike kuwaondoa ili kunusuru uharibifu usiendelee Zaidi katika maeneo hayo kwa ajili ya ustawi wa eneo hilo na nchi kwa ujumla.
Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri alisema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya madhara ya uvamizi wa hifadhi za mistu na baada ya elimu hiyo itawabidi watumie nguvu kwa watu wote ambao hawatakuwa tayari kubadilika.
Alisema sanjari na elimu hiyo alitoa wito wa kuimarisha nguvu katika matumizi majiko yanayotumia nishati kidogo nay ale ya gesi ili kunusu mistu nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack aliwataka watendaji wote kuanza kuwaondoa wavamizi wa vyanzo vya maji na mistu.
Aidha aliomba juhudi za usamabazaji wa gesi kwa ajili ya kupikia vijiji uongezwe ili kuwasaidia wananchi kuachana na matumizi ya mkaa na kuni ambazo zinachangia kumaliza mistu.
Naye Meneja wa Wakala wa Mistu Tanzania (TFS) Kanda ya Magharibi Valentine Msusa alisema wanayo orodha ya Ngitili zote zilikuwa zimehifadhi chini ya mradi HASHI na wanatarajia kukikabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya hatua zaidi.
Maadhimisho ya mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu isemayo Tanzania ya Kijani Inawezekana, Panda Miti kwa Maendeleo ya Viwanda.









No comments:
Post a Comment