TANGAZO


Tuesday, February 6, 2018

Bondia Muhammad Ali afungiwa miaka miwili

Boxing

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBondia Muhammad Ali amefungiwa kwa miaka miwili
Bondia Muhammad Ali, raia wa uingereza amefungiwa kwa miaka miwili kujihusisha na mchezo wa masubwi baada ya kushindwa vipimo vya dawa zilizokatazwa michezoni.
Ali mwenye miaka 21, alishindwa kufaulu vipimo alipokua anashiriki michezo ya dunia ya masubwi iliyofanyika nchini Morocco mwaka jana.
Bondia huyo alisimamishwa toka mwezi octoba mwaka jana na amefikia makubaliano ya kukubali adhabu hiyo na chama cha kimataifa cha mchezo wa ndondi. (AIBA).
Vipimo vinaonyesha bondia huyu amekuwa akitumia dawa aina ya Trenbolone, ambazo hutumika kukuza na kusisimua misuli na dawa hizo zimekatazwa michezoni na Wada.

No comments:

Post a Comment