TANGAZO


Sunday, January 7, 2018

Abiria waondolewa baada ya ndege mbili kugongana uwanja wa Toronto

Passenger photo shows fire on Sunwing plane's tail

Haki miliki ya picha@STEPHEN_BELFORD/VIA REUTERS
Image captionAbiria waondolewa baada ya ndege mbili kugongana uwanja wa Toronto
Ndege iliyokuwa imewasili Toronto iliondolewa abiria baada ya kugongwa na ndege nyingine iyokuwa bila abiria wakati ikiondolewa kutoka lango la kutokea abiria.
Shirika la ndege la WestJet lilisema kuwa ndege yake aina ya Boeing 737-800, iliyokuwa na abiria 168 na wahudumu sita ilikuwa inasubiri kuegeshwa kwenye lango la kutokea abiria wakati iligongwa na na ndege ya shirika la Sunwing.
Video ilionyesha moto karibu na mkia wa ndege ya Sunwing na abiria wa WestJet wakitiokea mlango wa dharura.
Ndege ya WesJet iliwasili Toronto ikitokea Cancun, Mexico na ilikuwa tayari imesimama wakati ajali hiyo ilitokea.
Huduma za dharura zilichukuliwa kwa haraka na abiria wakaondolewa.

No comments:

Post a Comment