Na Maharagande
AWALI, katika mabishano ambayo Jaji aliyatolea uamuzi Wakili Msomi Juma Nassoro amesema “Hatuwezi kuacha kumuuliza shahidi eti kwa sababu upande wa pili wanaumia na wanakereka na maswali anayouliza. Mhe. Nassoro alisisitiza kuwa “WATAKEREKA SANA SANA LAZIMA TUULIZE. MIMI NI MZARAMO UNAPOSEMA UNAKEREKA NAKUELEA SANA UNAMAANISHA NINI.”
Maswali alioulizwa Shahidi yalimbomoa Lipumba na uhalali wake, vikao FEKI alivyofanya na vilivyokosa akidi [Qoram]; Rejea MAHOJIANO YA WAKILI NA SHAHIDI Abubakar Hamis.
MAHOJIANO YA WAKILI NA SHAHIDI YALIKUWA KAMA IFUATAVYO:
NASSORO: Mtu ambaye sio mwanachama wala si Mwenyekiti wa Chama anaweza kuitisha kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la Chama?
SHAHIDI [ABUBAKAR KHAMISI BAKARI]: Hapana. Hawezi
NASSORO: Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi asipohudhuria vikao vya Baraza vilivyoitishwa na mtu ambaye sio mwanachama wala si Mwenyekiti ana lawama yoyote kikatiba?
SHAHIDI. Hana lawama kwasababu hicho kikao ni batili.
NASSORO: Maamuzi ya kikao cha Baraza kilichoitishwa na mtu ambaye sio Mwenyekiti wa CUF yana athari gani kikatiba na kisheria?
SHAHIDI: Hayana athari yoyote ni maamuzi batili.
NASSORO: Kuna mtu anajiita Mwenyekiti wa CUF anadai kaitisha kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF mara tatu (Oktoba, Novemba 2016 na January 2017) lakini wajumbe waliohudhuria ni 15 tu. JE MAAMUZI YA KIKAO HICHO YANA MAANA YOYOTE KIKATIBA?
SHAHIDI: Hayana maana yoyote sababu kikao hicho ni batili kwa sababu mbili; Moja, aliyekiitisha hana mamlaka lakini Pili, hata angekuwa na mamlaka kikao ni batili kwasababu akidi haikutimia (shahidi anarejea ibara ya 114 ya katiba) “Isipokuwa kama imeelezwa vinginevyo katika Katiba hii, kiwango cha wajumbe cha kuhalalisha kikao chochote cha Chama ni zaidi ya nusu ya wajumbe wote wa kikao hicho.”
NASSORO: kwa mujibu wa Katiba ya CUF ni chombo kipi kina mamlaka ya kujaza nafasi zilizo wazi za wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa?
SHAHIDI: kwa mujibu wa Ibara ya 81(2) ya Katiba ya CUF ni Baraza Kuu ndio lenye wajibu wa kujaza nafasi iliyowazi ya Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.
NASSORO: Sasa inadaiwa kuna wajumbe hawakuhudhuria vikao vitatu vya Baraza Kuu vilivyoitishwa na MTU ANAYEJIITA MWENYEKITI WA CUF na hivyo wajumbe hao kukoma kuwa wajumbe wa Baraza Kuu mwaka huu 2017. Swali Je nyinyi wajumbe wa Baraza Kuu mwaka huu mliwahi kukaa na kujaza hizo nafasi za hao wajumbe wanaodaiwa kuondolewa ujumbe kwa kutumia Ibara ya 81(2) ya Katiba ya CUF?
SHAHIDI: Hatujawahi kufanya hivyo KATU.
NASSORO: Kama hamjawahi kujaza hizo nafasi je hicho kikao kinachodaiwa kuitishwa na HUYO ANAYEJIITA MWENYEKITI kwa uelewa wako kilipata wapi hiyo akidi ya kuteua wajumbe wa Bodi ya Udhamini ilihali upande wa huyo anayejiita mwenyekiti una wajumbe 15 tu wa Baraza Kuu?
SHAHIDI: Akidi hawana na wala hicho kikao si halali na hivyo WASINGEWEZA KUFANYA KIKAO HALALI CHA KUTEUA WAJUMBE WA BODI YA UDHAMINI.
Kutokana na Mashambulizi makubwa ya kisheria yaliyokuwa yanafanywa na Wasomi Mawakili wa CUF, wakili wa Lipumba Majura Magafu aliiomba Mahakama kuahirisha Shauri hilo kutokana na kujisikia vibaya na kupata mshtuko ghafla [Blood Pressure-BP] na maumivu ya kichwa [Headache] hoja ambayo iliungwa mkono na Mashaka Ngole na Gabriel Malata. Kutokana na Likizo ya Mahakama [Court Vacation] iliyoanza tangu Tarehe 15 Disemba, 2017 Shauri hili limeahirishwa mpaka February 27 baada ya Wakili Msomi Fatma Karume kuomba isiwe February 6, 2018 kama ilivyopangwa awali. Ambapo Shahidi wa Pili Mhe. Joran Lwehabura Bashange ataanza kutoa ushahidi wake.
Imekusanywa na kuandaliwa;
Maharagande,
0715062577
December 24, 2017


No comments:
Post a Comment