TANGAZO


Friday, November 24, 2017

WAZIRI MWAKYEMBE: JITOKEZENI KUSAIDIA KUKUZA SEKTA YA MICHEZO

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza na waendeshaji wa michezo ya  kubahatishisha nchini (hawapo pichani)kuhusu kusaidia kuendeleza sekta ya michezo leo jijini Dar es Salaam kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Waendesha Michezo ya Kubahatisha nchini Bw.Dhiresh Kaba na Kulia Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu Uwanja wa Taifa Bw.Alex Nkenyenge. (Picha zote na Anitha Jonas - WHUSM)
Mwenyekiti wa Shirikisho la Waendesha Michezo ya Kubahatisha nchini Bw.Dhiresh Kaba (kulia) akitoa ahadi ya kuzungumza na shirikisho namna watakavyo changia kuendeleza sekta ya michezo nchini katika kikao cha waendeshaji wa michezo ya kubahatisha na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe(katikati) leo jijini Dar es Salaam kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.Yusuph Singo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe(watatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Makampuni ya Mchezo wa kubahatisha mara baada ya kikao kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam kujadili namna wadau hao watasaidia kukuza michezo nchini.

Na Anitha Jonas - WHUSM, Dar es Salaam
24/11/2017.
WAZIRIHabari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe amewataka wamiliki wa Kampuni za Michezo ya Kubahatisha kujitokeza kwa wingi na kusaidia ukuaji wa sekta ya Michezo.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo alipokutana na viongozi wa makapuni mbalimbali ya mchezo wa kubahatisha nchini  kwa lengo la kuzungumza nao kuhusu kuchangia sekta ya michezo kwa maendeleo ya taifa kama inavyofanyika katika mataifa mengine.

‘’Najua nyinyi ni wadau wakubwa wa michezo japo mchezo huu wa kubahatisha ni mgeni katika taifa letu ila ni mchezo unaokuwa kwa kasi hivyo ningependa kuona mnatoa ushirikiano katika kukuza sekta ya michezo kwa taifa kwani sekta ya hii imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo ukosefu wa fedha na miundombinu,’’alisema Dkt.Harrison Mwakyembe.

Pamoja na hayo Waziri huyo aliendelea kutoa shukrani kwa mchango uliyotolewa na moja ya Kampuni ya Mchezo wa kubahatisha ya Sportpesa kwa kutoa ufadhili wa kufanya matengenezo ya nyasi za uwanja wa Taifa zilizokuwa zimechakaa kufuatia maandalizi ya mashindano ya AFCON Under 17 ya 2019 yatakayofanyika nchini.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Shirikisho la Waendesha Michezo ya Kubahatisha (TSBA) Bw.Dhiresh Kaba aliahidi serikali kuwa shirikisho liko tayari kutoa  ushirikiano katika kuisaidia sekta ya michezo na sababu wanatambua umuhimu wa michezo kwa taifa.

‘’Naishukuru Serikali kwa kutupa nafasi ya kuweza kuchangia katika ya maendeleo ya michezo nchini sababu mchezo wetu unategema sana michezo na michezo ya nchini itakapopata mafanikio  itatusaidia na sisi kuongeza wigo wa mchezo huu wa kubahatisha,’’alisema Bw.Kaba.  

Hata hivyo michezo ya kubahatisha ni mmoja ya sekta inayokuwa kwa kasi nchini hivyo kupitia mchango wao wanaweza kusaidia kuboresha miundombinu ya michezo ambayo imekuwa na changamoto nyingi.

No comments:

Post a Comment