TANGAZO


Saturday, November 25, 2017

WAZIRI KAIRUKI: TUPAMBANE KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA

Baadhi ya wananchi na wadau wa maendeleo wakiwa katika maandamano maalum ya ufunguzi wa Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW)
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki akinyajua bango juu lenye ujumbe unaosema “Ukatili wa Kijinsia Unachelewesha Tanzania ya Viwanda” wakati akipokea Maandamano maalum ya ufunguzi wa Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki akiwaasa wadau na watanzania kujikita katika kupambana na ukatili wa kijinsia wakati akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Niabu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akieleza namna  Wizara inavyoshikiana na wadau na wananchi kupambana kuondoa ukatili wa kijinsia  katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Mkurugenzi wa Shirika la WILDAF Tanzania Dkt Judith Odunga akitoa salamu kwa niaba ya wadau katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leade’s Club Dar es Salaam Novemba 25, 2017. 
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki(kulia) akiteta jambo na Niabu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(kushoto) wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika Viwanja vya Leader’s club Kinondoni Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki akisaliamiana na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa Nchini Bw. Alvaro Rodriguez wakati wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25, 2017.  
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki akijadiliana jambo  na Mwakilishi wa Balozi wa Marekani nchini Bi Inmi Patterson wakti wa ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25, 2017.
Baadhi ya wadau na wananchi wakifuatlia hotuba ya Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) aliyemwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25, 2017. 
Baadhi ya wadau na wananchi wakifuatlia hotuba ya Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) aliyemwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25, 2017. 
Baadhi ya wadau na wananchi wakifuatlia hotuba ya Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki (hayupo pichani) aliyemwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leader’s Club Dar es Salaam Novemba 25, 2017. 
Waziri wa Nishati Mhe. Angellah Kairuki (watatu kushoto waliokaa )na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(katikati waliokaa) wakiwa katika picha ya pamoja wadau na waharakati wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uliofanyika katika viwanja vya Leade’s Club Dar es Salaam Novemba 25,2017. 

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
WATANZANIA wametakiwa kutumia nguvu zao katika kupambana na ukatili wa kijinsia katika maeneo yao ili kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia nchini.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini Mhe. Angellah Kairuki alipokuwa akimwakilisha Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Maadhimisho ya Siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia  nchini.

Mhe. Angellah Kairuki amesema kuwa kimsingi kiwango cha ukatili wa kijinsia nchini na dunia bado ni kubwa na kwa mujibu wa Taarifa ya Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria Tanzania ya mwaka 2015/2016 inaonesha kuwa wanawake 4 kati ya 10 wamewahi kukumbana na ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.

Ameongeza kuwa takwimu zinonesha kuwa asilimia 42 ya wanawake waliowahi kuolewa wamekumbana na ukatili wa wenza wao ama wa kimwili,au ukatili unaohusisha ngono.

“Nawaomba watanzania wenzangu  katika maeneo yenu pazeni sauti na kufanya kwa vitendo kupinga masuala ya ukatili wa kijinsia unaowakumba sana wanawake na watoto” alisema Mhe. Angellah.

Aidha kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Faustine Ndugulile amesema kuwa athari za ukatili wa kijinsia  ni kubwa sana katika Nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa kampeni hii ya Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia  hasa ilenge kuinua uelewa wa jamii na wadau mbalimbali kuhusu madhara ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

“Kampeni hii imekuja wakati muafaka na kwakuwa tatizo la ukatili wa kijinsia hapa nchini bado ni kubwa basi itasaidia kulitatua kwa jitihada za pamoja za Wadau na Serikali” alisema Mhe. Dkt. Ndugulile.

Naye Mkurugenzi wa WILDAF Tanzania Dkt. Judith Odunga ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wao katika kupambana na ukatili wa kijinsia na kuomba kufanyiwa kwa marekebisho ya baadhi ya Sheria ili ziende sambamba na kupinga ukatili wa kijinsia nchini.

Siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia uadhimishwa kila mwaka kuanzia Novemba 25 mpaka Desemba 10 na kwa mwaka 2017 Kauli mbiu inasema FUNGUKA! Ukatili Dhidi ya wanawake na Watoto haumwachi Mtu Salama: CHUKUA HATUA!

No comments:

Post a Comment