TANGAZO


Saturday, November 25, 2017

WAFANYAKAZI WA TAASISI YA OKOA MOYO WA MTOTO (SAVE A CHILD'S HEART (SACH) YA ISRAEL WAMTEMBELEA MTOTO JULIUS KAIJAGE MKOANI KAGERA ALIYEFANYIWA UPASUAJI WA MOYO NCHINI HUMO 2013

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu Salum akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa  Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a  Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel ambao walifika katika mkoa huo kwa ajili ya kumjulia hali na kufuatilia maendeleo  ya elimu ya  mtoto Julius  Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa Moyo nchini humo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu akiwa katika  kikao na wafanyakazi wa  Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel ambao walifika katika mkoa huo kwa ajili ya kumjulia hali na kufuatilia maendeleo ya elimu ya  mtoto Julius Kaijage  ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa Moyo nchini humo.

Mama Judy Shore  kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel ambaye anaishi nchini Marekani wakizungumza jambo na  mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa moyo nchini Israel. Mama Shore aliamua kuja nchini kumjulia hali mtoto Julius baada ya kupata taarifa za kupona kwake ugonjwa wa moyo. 
Mama Judy Shore na Tamar Shapira kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel wakizungumza jambo na  mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa moyo nchini humo. Wafanyakazi wa SACH walitembelea Mkoa wa Kagera kwa ajili ya kumjulia hali mtoto huyo.
Tamar Shapira kutoka Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart-SACH) ya nchini Israel akipokea zawadi ya kitenge kutoka kwa mtoto Julius Kaijage ambaye mwaka 2013 alifanyiwa upasuaji wa moyo nchini humo. Wafanyakazi wa SACH walitembelea mkoa wa Kagera kwa ajili ya kumjulia hali mtoto huyo. (Picha zote na JKCI)

No comments:

Post a Comment