TANGAZO


Saturday, November 25, 2017

TAARIFA YA CUF KUHUSU MAALIM SEIF KUWA MGENI RASMI MKUTANO WA WILAYA YA KILWA MKOANI LINDI

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad

KATBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif hamad, leo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi.

Katibu Mkuu ameambatana na Mkurugenzi wa Habari Mhe. Salim Bimani , Naibu Mkurugenzi wa Uchaguzi na Oganaizesheni Mhe. Shaweji Mketo , Afisa Habari Mhe. Anderson Ndambo, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Katibu wao Mhe. Juma K Hamad , Mratibu wa Matawi ya Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Rashid Abdallah na viongozi wengine waandamizi wa Chama.

Mkutano huo unatarajiwa kuanza mapema Asubuhi hii, na Maalim Seif anatarajiwa kutoa Hotuba nzito juu ya mustakbali wa Siasa Tanzania na muelekeo wake.

Haki sawa kwa wote
Maharagande,
NMHUMU.
25/11/2017

No comments:

Post a Comment