TANGAZO


Wednesday, November 22, 2017

Mkufunzi wa Sevilla apatikana na saratani

Wachezaji wa Sevilla baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Liverpool

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wa Sevilla baada ya kufunga bao la kusawazisha dhidi ya Liverpool
Klabu ya Sevilla imethibitisha kuwa mkufunzi wake amepatikana na ugonjwa wa saratani baada ya timu hiyo kutoka nyuma na kupata sare ya 3-3 dhidi ya Liverpool.
Vyombo vya habari vinasema kuwa Eduardo Berizzo ambaye anaugua saratani ya tezi dume aliwaelezea wachezaji wake kuhusu habari hiyo katika wakati wa mapumziko katika uwanja wa Estadio Ramon Sanchez Pizjuan.
Wachezaji wa Sevilla walimkimbilia Berizzo baada ya Guido Pizarro kufunga katika dakika za lala salama ili kusawazisha.
Taarifa ya klabu hiyo imemtakia mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 48 kupona kwa haraka.

No comments:

Post a Comment