TANGAZO


Saturday, November 18, 2017

Arsenal yainyamazisha Tottenham Hotspurs

Mechi kati ya Arsenal na Tottenham ambapo timu ya mkufunzi Wenger iliwalaza wapinzani wao wa jadi Tottenham

Haki miliki ya pichaPA
Image captionMechi kati ya Arsenal na Tottenham ambapo timu ya mkufunzi Wenger iliwalaza wapinzani wao wa jadi Tottenham
Arsenal ilifunga mabao mawili ya kipindi cha kwanza na kuwalaza wapinzani wao wa jadi mjini London Tottenham kwa mara ya kwanza katika mechi saba za ligi ya Uingereza.
Beki Shkrodan Mustafi alifunga kichwa kizuri kutoka kwa krosi iliopigwa na Mesut Ozil , lakini Spurs wanadai kwamba mpira wa adhabu uliopigwa baada ya Davinson kumchezea visivyo Alexis Sanchez ulikuwa uamuzi mkali.
The Gunners waliongeza bao la pili dakika tano baadaye , baada ya mshambuliaji wa Chile Sanchez kufunga krosi iliopigwa na Alexandre Lacazzette akiwa amekaribia goli.
Sanchez alikuwa na fursa ya kuongeza bao la tatu lakini shambulio lake likapanguliwa na Hugo Lloris.
Fursa nzuri ya wageni hao ilimwangukia kiungo wa kati Christian Eriksen katika kipindi cha kwanza lakini shambulio la kimo cha paka la raia huyo wa Denmark liligonga chuma cha goli huku kipa Petr Cech akiruka na kuokoa kichwa kilichopigwa na Eric Dier.
Ushindi huo sasa umeifanya Arsenal kupanda hadi katika nafasi ya tano katika jedwali la ligi wakiwa na pointi moja juu ya kikosi cha Mauricio Pochettino.

No comments:

Post a Comment